Andaa simu yako kwa urejelezi
Ukinunua simu mpya, au unataka kutupa simu yako, Nokia
inapendekeza a kwamba urejeleza simu yako. Kabla, ondoa maelezo
yote ya kibinafsi na yaliyomo kutoka kwenye simu yako.
Ondoa yaliyomo yote na rejesha mipangilio kwenye dhamani halisi
1. Cheleza yaliyomo unayotaka kuweka kwenye kadi ya kumbukumbu
inayotangamana au kompyuta inayotangamana.
2. Tamatisha simu na miunganisho yote.
3. Chagua mipangilio na rejesha mi. ya k'ani. > zote.
4. Charaza msimbo wa usalama.
5. Simu yako huzima na kisha kuwashwa tena. Kagua kwa makini
kwamba yaliyomo yote ya kibinafsi, kama vile majina, picha, muziki,
video, vitini, ujumbe, barua, maonyesho, michezo na programu
nyingine zilizosanidiwa zimeondolewa.
Yaliyomo na maelezo yanayohifadhiwa kwenye kadi ya kumbukumbu
au SIM kadi hayaondolewi.
85