Usalama
Soma maelekezo haya mepesi.
Kutoyafuata kunaweza kuwa hatari au
kinyume cha sheria. Kwa maelezo
zaidi, soma mwongozo kamili wa
mtumiaji.
ZIMA KATIKA MAENEO
YALIYOKATAZWA
Usiwashe kifaa wakati matumizi ya
simu zisizo na waya yamekatazwa au
wakati kinaweza kusababisha
mwingiliano au hatari, kwa mfano,
ndani ya ndege au hospitalini, au
karibu na vifaa vya matiba, mafuta,
kemikali, au maeneo yenye mlipuko.
Tii maagizo yote katika maeneo
yaliyozuiwa.
USALAMA BARABARANI
HUJA KWANZA
Tii sheria zote za mahali ulipo. Daima
iache mikono yako iwe huru
kuendesha gari. Kitu cha kuzingatia
kwanza unapoendesha gari unapaswa
kuwa usalama barabarani.
MWINGILIANO
Vifaa vyote visivyotumia
waya vina uwezekano wa kupata
mwingiliano, ambao unaweza kuathiri
utendaji kazi wake.
UTENGENEZWAJI
KITAALAM
Watu wenye ujuzi na sifa zinazotakiwa
tu ndio wanaweza kuweka au
kukarabati bidhaa hii.
LINDA UWEZO WAKO
WA KUSIKIA
Ili kuzuia uharibifu wa kusikia
unaowezekana, usisikilize katika sauti
ya juu kwa muda mrefu. Kuwa
mwangalifu wakati unashikilia kifaa
chako karibu na sikio wakati kipasa
sauti kinatumika.
Maagizo mahsusi ya nduni
1
Muhimu: Kifaa hiki kimeundwa
ili kutumiwa na SIM kadi wastani tu
(angalia mfano). Utumizi wa SIM kadi
zisizotangamana huenda kukaharibu
kadi au kifaa, na huenda kukaharibu
data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Tafadhali shaurinan na opereta wa
rununu yako kwa utumizi wa SIM kadi
ambayo ina mkato wa mini-UICC.
2
Tahadhari: Wakati mfumo wa
angani umeamilishwa, huwezi kupiga
au kupokea simu zozote, pamoja na
simu za dharura, au kutumia vitendaji
vingine ambavyo vinahitaji kuwepo
95
kwa mtandao. Kupiga simu, amilisha
mfumo mwingine.
3 Kifaa chako kinaweza kuwa na
antena ya ndani na ya nje. Jiepushe
kugusa eneo la antena bila sababu
wakati antena inapopitisha au
kupokea. Ugusaji antena huathiri
ubora wa mawasiliano na unaweza
kusababisha kiwango kikubwa zaidi
cha nishati wakati wa utendaji kazi na
inaweza kupunguza uhai wa betri.
Tumia tu kadi za kumbukumbu
zinazoendana zilizoidhinishwa na
Nokia kwa ajili ya kutumiwa na kifaa
hiki. Kadi zisizoendana zinaweza
kuharibu kadi na kifaa na kuharibu
data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Kifaa chako kinakubali kadi za
microSD zenye uwezo wa hadi 32 GB.
Muhimu: Usiondoe kadi ya
kumbukumbu wakati programu tumizi
inaitumia. Kufanya hivyo kunaweza
kuharibu kadi ya kumbukumbu na
kifaa na kuharibu data iliyohifadhiwa
kwenye kadi.
4
Muhimu: Epuka kukwaruza
kizinza cha kuguswa. Kamwe usitumie
kalamu, penseli, au kitu kingine
chenye ncha kali kuandika kwenye
kizinza cha kuguswa.
Kusikiliza redio, unahitaji kuungnaisha
Kifaa kinachoendana cha kuvaa
kichwani kwenye kifaa. Kifaa cha
kichwa hufanya kazi kama antena.
Huduma za mtandao wa jamii ni
huduma za wahusika wa tatu na
hazitolewi na Nokia. Kagua mipangilio
ya faragha ya huduma ya mtandao wa
jamii uanotumia kwa kuwa unaweza
kushiriki maelezo na kikundi kikubwa
cha watu. Masharti ya matumizi ya
huduma ya mtandao wa jamii
hutumika ili kushiriki maelezo kwa
huduma hiyo. Jifahamishe na
masharti ya utumizi na desturi za siri
za huduma hiyo.
Utumiaji wa huduma za mtandao wa
jamii unahitaji usaidizi wa mtandao. Hii
huenda ikajumuisha upitishaji wa
viwango vikubwa vya data na gharama
za trafiki ya data husika. Kwa maelezo
kuhusu gharahama ya upitishaji data,
wasiliana na mtoa huduma wako.
Huenda programu tumizi ya Jamii
isipatikane katika maeneo yote. Nduni
zile zinazokubaliwa na huduma ya
mtandao wa jamii pekee zinapatikana.
96
5 Unaweza kutuma ujumbe wa
maandishi ambayo ni refu zaidi ya
kizuizi cha vibambo kwa ujumbe
mmoja. Ujumbe mrefu zaidi utatumwa
kama ujumbe wa pili au zaidi. Mtoa
huduma wako anaweza kudai malipo
kadri inavyotakiwa.
Herufi au alama ambazo zina lafudhi,
alama zingine, au chaguo zingine za
lugha huchukua nafasi kubwa zaidi,
hivyo kupunguza idadi ya herufi
zinazoweza kutumwa kwenye ujumbe
mmoja.
6 Kama kipengee ulichoingiza
katika ujumbe wa medianuwai ni
kikubwa sana kwa mtandao, huenda
kifaa kikapunguza saizi kiotomati.
7 Vifaa vinavyotangamana tu
ndivyo vinavyoweza kupokea na
kuonyesha ujumbe wa medianuwai.
Huenda ujumbe ukaonekana tofauti
katika vifaa tofauti.
8 Kutumia huduma hiyo au kupakua
yaliyomo huenda yakasababisha
uhamishaji wa viwango vikubwa vya
data, ambayo inaweza kusababisha
gharama ya trafiki ya data.
Ujumbe wa picha huenda ukaonekana
tofauti katika vifaa tofauti.
Usiunganishe bidhaa ambazo
zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii
inaweza kuharibu kifaa. Usiunganishe
chanzo chochote cha stima kwa
Kiunganisha Nokia AV. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au kifaa
chochote cha kichwa kwa Kiunganisha
Nokia AV, kando na zile
zilizoidhinishwa na Nokia kwa
kutumiwa na kifaa hiki, kuwa makini
sana na viwango vya sauti.
Muhimu: Kabla ya kushiriki eneo
lako, daima zingatia kwa makini
unashirikiana na nani. Kagua
mipangilio ya siri ya huduma ya
mtandao wa jamii unaotumika, kwa
kuwa unaweza kushiriki eneo lako na
kikundi kikubwa cha watu.
9 Kama betri imeishiwa chaji
kabisa, inaweza kuchukua dakika
kadhaa kabla kiashirio cha kuchaji
kuonyeshwa au kabla simu zozote
kuweza kupigwa.
Kumbuka kufuata mahitaji yoyote
husika ya usalama.
Kuzima arifu kutoka kwenye
programu ya mtandao wa jamii,
kwenye skrini ya programu, chagua
Arifu > > mipangilio.
97
Huduma za mtandao na
gharama
Kifaa chako kimeidhinishwa kwa
matumizi na Mitandao ya WCDMA 850,
900, 1700, 1900, 2100, na HSPA
EGSM 850, 900, 1800, 1900 MHz .
Kutumia kifaa hiki, unahitaji kujiunga
na mtoa huduma.
Kutumia baadhi ya vipengele na
kupakua yaliyomo kwenye kifaa chako
uhitaji muunganisho wa mtandao na
huenda kukasababisha gharama ya
trafiki ya data. Baadhi ya nduni za
bidhaa uhitaji usaidizi kutoka kwa
mtandao, na huenda ukahitaji
kujiunga.
Kuhudumia kifaa chako
Shughulikia kifaa chako, betri, chaja
na vifaa vya ziada kwa uangalifu.
Mapendekezo yafuatayo yatakusaidia
kulinda matakwa ya dhamana yako.
•
Usitumie au kuhifadhi kifaa
chako kwenye maeneo yenye
vumbi au uchafu. Sehemu zake
zinazosogea na vijenzi vya
elektroniki vinaweza kuharibika.
•
Usihifadhi kifaa kwenye hajijoto
ya juu au ya chini. Joto la juu
linaweza kufupisha maisha ya
vifaa vya elektroniki, kuharibu
betri, na kukunja au kuyeyusha
aina fulani za plastiki.
•
Usihifadhi kifaa kwenye halijoto
baridi. Wakati kimerudi kwenye
joto lake la kawaida,
unyevunyevu unaweza
kutengenezeka ndani ya kifaa,
ambao unaweza kuharibu bodi
za saketi za eletroni.
•
Usijaribu kufungua kifaa zaidi ya
jinsi ilivyoelekezwa kwenye
mwongozo huu.
•
Antena, kufanya mabadiliko au
kuweka viambatisho
visivyoidhinishwa kunaweza
kuharibu kifaa hiki na kunaweza
kukiuka sheria zinazoendana na
vifaa vya redio.
•
Usiangushe, kugonga au
kutikisa kifaa hiki. Kushika
vibaya kunaweza kuvunja bodi
za umeme na ufundi wa ndani.
•
Tumia kitambaa laini, kisafi na
kikavu kusafisha uso wa kifaa
hiki.
•
Usipake rangi kifaa. Rangi
inaweza kuziba sehemu zake
zinazosogea na kuzuia utendaji
kazi mzuri.
98
•
Zima kifaa na uondoe betri mara
kwa mara kwa utendakazi bora.
•
Weka kifaa chako mbali na
sumaku au maeneo ya sumaku.
•
Ili kuweka data yako muhimu
salama, ihifadhi angalau katika
maeneo mawili tofauti, kama
vile kifaa chako, kadi ya
kumbukumbu, au kompyuta au
andika maelezo muhimu.
Wakati wa utendajikazi kwa muda
mrefu, kifaa kinaweza kuwa na joto.
Katika hali nyingi, hii ni kawaida. Kama
unashuku kifaa hakifanyi kazi
sawasawa, kipeleke kwenye kitengo
cha mtengenezaji aliyeidhinishwa
kilicho karibu.
Uchakataji upya
Daima rudisha bidhaa zako za
elektroniki, betri na nyezo za kifurushi
zilizotumiwa kwa maeneo maalum ya
ukusanyaji. Kwa njia hii utasaidia
kuzuia utupataji taka usiodhibitiwa na
kukuza uchakataji upya wa nyenzo.
Kagua jinsi ya kuchakata upya bidhaa
zako za Nokia www.nokia.com/
recycling.
Alama ya pipa iliyo na mkato
Alama ya pipa iliyo na mkato kwenye
bidhaa, maandishi, au kifurushi chako
hukukumbusha kwamba bidhaa zote
za elektroniki, betri, na vilikimbizi
umeme lazima zipelekwe kwenye
mkusanyiko tofauti wakati bidhaa
inapokwisha. Hitaji hili linatumika
katika Jumuiya ya Ulaya. Usitupe
bidhaa hizi kama takataka
zisizochambuliwa za manispaa. Kwa
taarifa zaidi juu ya mazingira, angalia
mfumo wa Mazingira wa bidhaa
kwenye www.nokia.com/ecoprofile.
Kuhusu Usimamiaji haki za
Dijito (‘Digital rights
management’)
Unapokuwa ukitumia kifaa hiki, tii
sheria zote na heshimu utamaduni wa
wenyeji, uhuru binafsi wa mtu na haki
halali za wengine, ikiwemo hakimiliki..
Kinga za hakimiliki zinaweza kukuzuia
dhidi ya kunakili, kurekebisha au
kuhamisha picha, muziki na vitu
vingine.
Wamiliki wa vilivyomo wanaweza
kutumia aina tofauti za teknolojia za
usimamiaji haki za kidijito (‘digital
99
rights management’ - DRM) kulinda
haki zao za ubunifu, zikiwemo
hakimiliki. Kifaa hiki kinatumia aina
anuai za maunzi laini ya DRM ili kuingia
kwenye vitu vinavyolindwa na DRM.
Kwa kutumia kifaa hiki unaweza
kufikia vilivyomo vilivyolindwa na OMA
DRM 2.0 & 2.1. Ikiwa baadhi ya maunzi
laini ya DRM yameshindwa kulinda
vilivyomo, wamiliki wa vilivyomo
wanaweza kuomba kwamba uwezo wa
maunzi laini hayo ya DRM ya kuingia
kwenye vitu vipya vinavyolindwa na
DRM ubatilishwe. Ubatilishwaji huo
unaweza pia kuzuia uwekwaji upya wa
vitu vinavyolindwa na DRM ambavyo
tayari viko kwenye kifaa chako.
Ubatilishwaji wa maunzi laini hayo ya
DRM hauathiri matumizi ya vitu
vinavyolindwa na aina nyingine za
DRM au matumizi ya vitu visivyolindwa
na DRM.
Vitu vinavyolindwa na usimamiaji haki
za kidijito (DRM) huja na leseni ambayo
huainisha haki zako za kutumia
vilivyomo.
Ikiwa kifaa chako kina yaliyomo
yaliyolindwa ya OMA DRM, ili
kucheleza leseni zote na yaliyomo,
tumia kitendaji cha chelezo kwenye
Nokia Suite.
Namna nyingine za uhamishaji huenda
zisihamishe leseni ambazo zinahitaji
kurejeshwa na vilivyomo ili uweze
kuendelea na matumizi ya vitu
vinavyolindwa na OMA DRM- baada ya
kumbukumbu ya kifaa kufomatiwa.
Unaweza pia kuhitaji kurejesha leseni
ikiwa faili kwenye kifaa chako
zitaharibika.
Kama kifaa chako kina vitu
vinavyolindwa na WMDRM, leseni na
vilivyomo vikipotea kama
kumbukumbu ya kifaa ikifomatiwa.
Unaweza pia kupoteza leseni na
vilivyomo ikiwa mafaili kwenye kifaa
chako kikiharibika. Kupoteza leseni au
vilivyomo kunaweza kupunguza
uwezo wako wa kutumia vilivyomo
vilevile kwenye kifaa chako tena. Kwa
taarifa zaidi, wasiliana na mtoa
huduma wako.
Vidokezo na Matoleo
Ili kukusaidia kunufaika kabisa na simu
yako na huduma, utapokea ujumbe
maalum wa maandishi bila malipo
kutoka Nokia. Ujumbe utakuwa na
vidokezo na mbinu na usaidizi.
Kuzuia upokeaji wa risala, chagu
mipangilio > akaun. ya Nokia >
Vidokezo na Matoleo.
100
Ili kutoa huduma iliyofafanuliwa hapa
juu, nambari yako ya simu ya rununu,
nambari tambulishi ya simu yako, na
vitambuaji vingine vya usajili wa
rununu hutumwa kwa Nokia wakati
unapotumia simu kwa mara ya
kwanza. Baadhi au maelezo yote
huenda pia yakatumwa kwa Nokia
wakati unasasisha programu. Huenda
maelezo haya yakatumiwa kama
ilivyobainishwa katika sera ya usiri,
inayopatikana katika www.nokia.com.
Betri na chaja
Maelezo ya betri na chaja
Kifaa chako kimekusudiwa kutumiwa
na betri inayoweza kuchajiwa upya ya
BL-4U . Nokia inaweza kutengeneza
modeli za ziada za betri zipatikane
kwa kifaa hiki. Daima tumia betri halisi
za Nokia.
Kifaa hiki kimekusudiwa kutumika
kinapopokea umeme kutoka kwa
chaja zifuatazo: AC-11 . Namba asili ya
modeli ya chaja ya Nokia huenda
ikatofautiana kulingana na aina ya
chomeka, inayotambuliwa na E, X, AR,
U, A, C, K, B, au N.
Betri inaweza kuchajiwa na
kuondolewa chaji hata mara mia, lakini
hatimaye itachoka. Wakati muda wa
kuongea na muda wa kusubiri
unaonekana wazi kuwa mfupi kuliko
kawaida, badilisha betri.
Usalama wa betri
Daima zima na ung'oe chaja kabla ya
kuondoa betri. Unapochopoa chaja au
kifaa chochote cha ziada, kamata na
uvute plagi na siyo waya.
Wakati chaja yako haitumiki, ichomoe
kwenye plagi ya umeme na kwenye
kifaa. Usiache betri iliyochajiwa kabisa
ikiwa imeunganishwa kwenye chaja,
kwa sababu uwekaji wa chaji ya ziada
kunaweza kufupisha maisha ya betri.
Ikiachwa bila kutumika, betri iliyokuwa
imejaa chaji itapoteza chaji yake kadri
muda unavyopita.
Daima jaribu kuweka betri kwenye
halijoto kati ya 15°C na 25°C (59°F na
77°F). Halijoto ya juu sana hupunguza
uwezo na uhai wa betri. Kifaa chenye
betri moto au baridi kinaweza
kisifanye kazi kwa muda.
Mkato wa umeme unaweza kutokea
kwa bahati mbaya kama kitu cha
chuma kweneye betri, kwa mfano,
ukibeba betri ya ziada mfukoni. Mkato
wa umeme kwenye temino huweza
kuharibu betri au hicho
kinachounganisha.
Usitupe betri zilizokwishatumika
kwenye moto kwa sababu zinaweza
101
kulipuka. Tupa betri kwa kufuata
sheria za mahali ulipo. Rejeleza betri
pale inapowezekana. Usitupe kama
takataka za kawaida za nyumbani.
Usichanechane, kukata, kufungua,
kugongesha, kukunja, kuharibu, au
kupasua seli au betri. Katika tukio la
betri kuvuja, usiruhusu umaji wa betri
kugusana na ngozi au macho. Hii
ikifanyika, osha maeneo yaliyoathirika
mara moja na maji, au tafuta msaada
wa kitabibu.
Usirekebishe, kutengeneza tena,
kujaribu kuingiza vitu geni kwenye
betri, au kuingiza au kuweka wazi kwa
maji au umiminiko mwingine. Betri
zinaweza kulipuka kama zimeharibika.
Tumia betri na chaja kwa matumizi
yaliyokusudiwa tu. Utumiaji mbaya, au
utumiaji wa betri au chaja
isiyotangamana inaweza kuleta hatari
ya moto, mlipuko, uvujaji, au hatari
zingine, na huenda ukabatilisha kibali
chochote au waranti. Kama unaamini
betri au chaja imeharibika, ipeleke kwa
kituo cha huduma ifanyiwe uchunguzi
kabla ya kuendelea kuitumia. Kamwe
usitumie betri au chaja yoyote
iliyoharibika. Tumia chaja ndani ya
nyumba tu.
Taarifa ya nyongeza kuhusu
usalama
Piga simu ya dharura
1
Hakikisha kifaa kimewashwa.
2
Angalia kama kuna mawimbi ya
simu ya kutosha. Huenda pia
ukahitaji kufanya yafuatayo:
• Ingiza SIM kadi katika kifaa.
• Zima vizuizi vya simu katika
kifaa chako, kama vile uzuiaji
simu, upigaji uliopangwa, au
kikundi maalum cha mtumiaji.
• Hakikisha mfumo wa angani
umeamilishwa.
• Kama skrini ya kifaa na vitufe
vimefungwa, vifungue.
3
Bonyeza kitufe cha kukata kwa
kurudia, hadi skrini kaya
ionyeshwe.
4
Ili kufungua kipigaji simu,
chagua .
5
Charaza namba halali ya dharura
ya eneo lako la sasa. Namba za
simu ya dharura hutofautiana
kimaeneo.
6
Bonyeza kitufe cha kupiga simu.
7
Toa maelezo yanayofaa kwa
usahihi kama iwezekanavyo.
Usikate simu mpaka upewe
ruhusa ya kufanya hivyo.
102
Muhimu: Amilisha simu zote za
selula na za tovuti, kama kifaa chako
kinakubali simu za tovuti. Kifaa
kitajaribu kupiga simu ya dharura kwa
mitandao ya selula na kupitia mtoa
huduma wako wa simu ya tovuti ikiwa
zote zimeakishwa. Unganisho katika
hali zote haziwezi kuhakikishwa.
Kamwe usitegemee kifaa chochote
kisichotumia waya pekee kwa
mawasiliano muhimu kama dharura za
tiba.
Watoto wadogo
Kifaa chako na viboreshaji vyake sio
sesere. Vinawezakuwa na sehemu
ndogo ndogo. Viweke mbali na watoto
wadogo wanapoweza kufika.
Vifaa vya matibabu
Utumiaji wa kifaa kinachotoa mawimbi
ya redio, ikiwa ni pamoja na simu
zisizotumia waya, kunaweza
kuingiliana na utendakazi wa vifaa vya
kitabibu ambavyo havijalindwa
kikamilifu. Mwone daktari au
mtengenezaji wa kifaa hicho cha
kitabibu kujua kama vimelindwa
kikamilifu dhidi ya nishati ya mawimbi
ya redio ya nje.
Vifaa vya matibabu
Watengenezaji wa vifaa vya matibabu
hupendekeza utenganisho wa angalau
sentimeta 15.3 (inchi 6) kati ya kifaa
kisichotumia waya na kifaa cha
matibabu mwilini, kama vile
kirekebisha mapigo ya moyo na vifaa
vingine vinavyohusiana na moyo ili
kuepuka uwezekano wa mwingiliano
na kifaa hicho cha kimatibabu. Watu
ambao wana vifaa kama hivyo
wanapaswa:
•
Daima weka kifaa kisichotumia
waya kwa umbali wa sentimeta
15.3 (inchi 6) kutoka kwa kifaa
cha matibabu.
•
Usibebe kifaa kisichotumia
waya katika mfuko wa shati.
•
Shikilia kifaa kisichotumia waya
kwenye sikio kando na kifaa cha
matibabu.
•
Zima kifaa wailesi kama kuna
sababu yoyote ya kushuku
kwamba mwingiliano
unafanyika.
•
Fuata maagizo ya mtengenezaji
kwa kifaa cha matibabu mwilini.
Ikiwa una maswali yoyote kuhusu
kutumia kifaa chako kisichotumia
waya na kifaa cha matibabu mwilini,
wasiliana na mtoa huduma wako wa
afya.
103
Vifaa vya kusaidia kusikia
Tahadhari: Wakati unatumia kifaa
cha kuvaa kichwani, uwezo wako wa
kusikiliza sauti za nje unaweza
kuathirika. Usitumie kifaa cha kuvaa
kichwani mahali ambapo kinaweza
kuhatarisha usalama wako.
Baadhi ya vifaa visivyotumia waya
vinaweza kuingiliana na baadhi ya
vifaa vya kusaidia kusikia.
Nikeli
Uso wa kifaa hiki hakina nikeli.
Linda kifaa chako dhidi ya vitu
vyenye madhara
Kifaa chako kinaweza kupata virusi na
vitu vingine vyenye madhara. Chukua
tahadhari zifuatazo:
•
Kuwa mwangalifu wakati wa
kufungua ujumbe. Huenda
zikawa na programu mbaya au
yenye kudhuru kifaa au
kompyuta yako.
•
Kuwa mwangalifu wakati
unakubali maombi ya
muunganisho, unapovinjari
tovuti, au kupakua yaliyomo.
Usikubali miunganisho ya
Bluetooth kutoka kwenye
vyanzo usivyoviamini.
•
Sakinisha na tumia huduma na
programu kutoka vyanzo
ambazo unaziamini tu na
ambazo hutoa usalama na
ulinzi.
•
Sakinisha kizuia virusi na
programu zingine za usalama
kwenye kifaa chako na
kompyuta yoyoye
iliyounganishwa. Tumia tu
programu moja ya kinga virusi
kwa wakati mmoja. Kutumia
zaidi ya moja huenda kukaathiri
utendakazi na utumizi wa kifaa
na/au kompyuta.
•
Ikiwa unafikia vialamisho
vilivyosakinishwa mapema na
viungo kwa tovuti vya mhusika
wa tatu, chukua tahadhari
zinazohitajika. Nokia
haiidhinishi wala kutoa dhamana
kwa ajili ya tovuti hizo.
Mazingira ya kutumia
Kifaa hiki kinaafikia maongozi ya
ujiwekaji wazi wa masafa ya redio
katika mkao wa utumizi wa kawaida
kwenye sikio au angalau sentimita 1.5
(inchi 5/8) mbali na mwili. Kikasha
chochote cha kubebea, kishikiza
kwenye mkanda, au kishikizi cha
matumizi ya kuvaliwa mwilini,
kinatakiwa kisiwe na chuma na
104
kinatakiwa kuweka bidhaa hii angalau
umbali uliotajwa hapo juu kutoka
kwenye mwili wako.
Kutuma faili za data au ujumbe uhitaji
unganiko na mtandao wenye ubora wa
hali ya juu. Faili za data au ujumbe
zinaweza kucheleweshwa hadi
unganisho huo upatikane. Fuata
maagizo ya umbali wa kutenganisha
hadi upitisho ukamilike.
Magari
Mawimbi ya redio (RF) yanaweza
kuathiri mifumo ya eletroni iliyo ndani
ya gari ambayo imewekwa vibaya au
haijalindwa kikamilifu, kwa mfano
utemaji wa mafuta kieletroniki;
kufunga breki kieletroniki, kidhibiti
mwendo kieletroniki, na mifuko ya
hewa. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na
mtengenezaji wa gari lako au vifaa
vyake.
Watu wenye ujuzi na sifa zinazotakiwa
tu ndio wanaweza kukarabati au
kuweka kifaa ndani ya gari.
Usakinishaji au huduma mbaya
inawezakuwa hatari na inaweza
kubatilisha waranti yako. Hakikisha
mara kwa mara kwamba vifaa vyote
visivyotumia waya ndani ya gari
vimefungwa vizuri na vinafanya kazi
sawasawa. Usihifadhi au kubeba
vimiminika vinavyoweza kuwaka, gesi
au vitu vyenye kulipuka kwenye
kichumba kimoja na kifaa hiki, sehemu
zake au vifaa vyake vya ziada.
Kumbuka kwamba mifuko ya hewa
hujaa hewa kwa nguvu kubwa.
Usiweke kifaa chako au viboreshaji
kwenye eneo ambalo mfuko wa hewa
hutumika.
Mazingira yenye uwezekano wa
milipuko
Zima kifaa chako katika eneo lolote
lenya mazingira yanayoweza kulipika,
kwa mfano karika na pampu za mafuta
katika vituo vya mafuta. Cheche katika
maeneo kama hayo zinaweza
kusababisha mlipuko au moto
unaoweza kuleta majeraha ya mwili au
kifo. Fuata masharti kwenye vituo vya
mafuta, maeneo ya kuhifadhi na
kugawia mafuta, viwanda vya kemikali
au mahali ambapo shughuli za ulipuaji
zinaendelea kufanyika. Maeneo yenye
mazingira yenye uwezekano wa
milipuko mara nyingi lakini si mara
zote yanakuwa na alama zilizo wazi.
Zinajumuisha maeneo ambapo
unaweza kushauriwa kuzima injini ya
gari lako, chini ya sitaha kwenye boti,
uhamishaji kemikali au suhula za
kuhifadhi, na ambapo hewa ina
kemikali au chembechembe kama vile
nafaka, vumbi au poda ya chuma.
Unapaswa kuwasiliana na
105
watengenezaji wa magari
yanayotumia mafuta aina ya gesi oevu
ya petroli iliyoyeyushwa (kama vile
propeni au buteni); ili kuamua ikiwa
kifaa hiki kinaweza kutumiwa vizuri
katika maeneo yao.
Habari ya utoaji cheti (SAR)
Kifaa hiki cha mkononi kinatimiza
maelekezo yanayohusu ujiwekaji
wazi kwa mawimbi ya redio.
Kifaa chako cha mkononi ni transmita
na kipokezi cha redio. Imesanifiwa
isizidi viwango vya juu vya ujiwekaji
wazi kwa nishati ya frikwensi za redio
vilivyopendekezwa na maelekezo ya
kimataifa. Maelekezo haya
yalitayarishwa na shirika huru la
kisayansi ICNIRP na yanajumuisha
viwango vya tahadhari ya ziada
iliyowekwa kuhakikisha usalama wa
watu wote, bila kujali umri wala afya.
Maelekezo ya ujiwekaji wazi kwa ajili ya
vifaa vya mkononi hutumia kizio cha
kipimo kijulikanacho kama Kiwango
Maalum cha Ufyonzaji ( ‘Specific
Absorption Rate, au SAR’ ). Kiwango
cha juu cha SAR kilichoelezwa kwenye
maelekezo hayo ya ICNIRP ni 2.0 wati/
kilogramu (W/kg) kilichotokana na
wastani wa gramu 10 za tishu. Vipimo
kwa ajili ya SAR hufanyika kwa kutumia
mikao ya matumizi ya kawaida na kifaa
kikiwa kinatumika kwa kiwango chake
cha juu cha nguvu kilichosajiliwa
kwenye frikwensi za bendi zote
zilizojaribiwa. Kiwango halisi cha SAR
cha kifaa wakati kinatumika kinaweza
kuwa chini ya kiwango cha juu kabisa
kwa sababu kifaa kimesanifiwa
kutumia kiasi kile cha nguvu
inayohitajika tu kufika kwenye
mtandao. Kiasi hicho hubadilika
kutegemea sababu kadhaa kama vile
ukaribu wa kituo cha mtandao.
Kiwango cha juu cha SAR kwenye
maelekezo ya ICNIRP wakati wa
kutumia kifaa karibu na sikio ni W/kg
1.37 .
Matumizi ya vifaa vya ziada yanaweza
kusababisha viwango tofauti vya SAR.
Viwango vya SAR vinaweza
kutofautiana kutegemea matakwa ya
nchi kuhusu utoaji taarifa na upimaji
na bendi ya mtandao. Taarifa zaidi
kuhusu SAR inaweza kupatikana chini
ya taarifa ya bidhaa kwenye
www.nokia.com.