
Kuhusu visasisho vya programu ya simu
Kuwa katika hali sawa na mdundo - sasisha programu ya simu yako ili
upate vipengee vipya na vilivyoboreshwa vya simu yako. Kusasisha
programu kunaweza pia kuboresha utendakazi wa simu yako.
Inapendekezwa kwamba ucheleze data zako za kibinafsi kabla ya
kusasisha programu ya simu yako.
Tahadhari:
Ukiingiza kisasishaji cha maunzi laini, huwezi kutumia kifaa hicho, hata kupiga simu za
dharura, mpaka usasishaji ukamilike na kifaa kiwashwe upya.
Kutumia huduma hiyo au kupakua yaliyomo huenda yakasababisha
uhamishaji wa viwango vikubwa vya data, ambayo inaweza
kusababisha gharama ya trafiki ya data.
Kabla ya kuanzisha kusasisha, unganisha chaja au hakikisha betri ya
kifaa ina nishati ya kutosha.
Baada ya kusasisha, maagizo katika kiongozi cha mtumiaji huenda
yasiwe yamesasishwa. Huenda ukapata kiongozi cha mtumiaji
kilichosasishwa kwenye www.nokia.com/support.
89