
Wapigie simu watu kadhaa kwa wakati sawa
Unataka kuwaelezea marafiki wako habari njema? Ukiwa na simu ya
mkutano, unaweza kuwapigia kwa urahisi watu kadhaa kwa wakati
mmoja, kwa hivyo kukuepusha dhidi ya kupigia simu kila mmoja.
Simu ya mkutano ni huduma ya mtandao. Kwa upatikanaji, wasiliana
na mtoa huduma wako wa mtandao.
1. Piga simu ya kwanza.
2. Ukiwa kwenye simu, chagua chaguzi > simu mpya > Simu.
3. Charaza namba ya simu, kisha uchague SIMU, au chagua TAFUTA
na jina. Simu ya kwanza husubiri hadi uunganishe simu ya mkutano.
4. Wakati unaweza kuongea na mpigaji wa pili, chagua chaguzi >
mkutano. Unaweza kuongeza simu zaidi kwenye mkutano.
Kidokezo: Ili kuongea kibinafsi na mpigaji simu katika simu ya
mkutano, chagua chaguzi > simu ya kibinafsi na namba. Simu ya
mkutano husubiri. Ili kurudi kwenye simu ya mkutano, chagua
chaguzi > mkutano.
5. Ili kukatisha simu ya mkutano, bonyeza
.
29