Kagua barua yako ya sauti
Je, uliruhusu simu zako zikaenda kwa barua ya sauti wakati hukuweza
kujibu? Sikiliza ujumbe ambao watu wamewacha kwa wakati wako.
Sanidi barua yako ya sauti
Ili kutumia barua ya sauti, huenda ukahitaji kujisajili na huduma. Kwa
maelezo zaidi juu ya huduma hii ya mtandao, wasiliana na mtoa
huduma wa mtandao wako.
Kabla ya kutumia kasha lako la sauti, pata namba yako ya kasha la
sauti kutoka kwa mtoa huduma wa mtandao wako. Kagua dhibitisho
lako au wavuti ya usaidizi ya mtoa huduma wa mtandao wako.
1. Chagua mipangilio > simu > mipangilio zaidi > barua za sauti na
na. ya kasha sauti..
2. Charaza namba yako ya kasha la sauti, kisha chagua Sawa.
Sikiliza barua yako ya sauti wakati umekosa simu
1. Chagua arifu ya ujumbe mpya kwenye skrini kaya.
2. Chagua chaguzi > mpi. si. mtumaji.
Sikiliza barua yako ya sauti baadaye
Chagua simu, kisha bonyeza na ushikilie 1.
48